TANRIKS MIAKA KUMI 09 FEBRUARI 2022
Tanriks inawakaribisha Diaspora na Umma kushiriki pamoja katika tafrija ya kusherekea miaka kumi ya tangu kuanzishwa kwake. Tafrija itafanyika machi 26 2022 katika ukumbi wa SOFIELUNDS FOLKET HUS, ROLFSGATAN 16 MALMÖ kuanzia saa kumi na mbili joini baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa Tanriks 2022.
Ada kwa mshiriki ni SEK 200, kwa huduma za Chakula , Kinywaji, Ukumbi na burudani, Unaweza kulipia Ada ya ushiriki wako kupitia SWISH NO: 1230227694- TANZANISKARIKSFÖRBUNDET AU KWA MALIPO YA BANK Ukamilishapo malipo tafadhari mjulishe mtunza hazina kupitia simu namba +46760558079. Tafadhari kumbuka kuambatanisha Jina lako kamili na namba ya mawasiliano kwa taarifa zaidi, taadhali ya Uviko19 itazingatiwa.
Usomapo taarifa hii unaweza kuwajulisha na wengine, wote mnakaribishwa.,
TANRIKS INAWALETA WATU WOTE PAMOJA
Zubeda Tihakana
Mtunza Hazina
Tanriks