TANZANISKA RIKSFÖRBUNDET
Tanzaniska riksförbundet bevarar, utvecklar och presenterar vår östafrikanska nationella, språkliga och kulturella identiteten inom ramen för ett multikulturellt svenskt samhälle.
Vårt mål är att främja integration och demokrati och motverka rasism och utanförskap. Välkommen till oss!
UTANGULIZI KATIBA YA TANRIKS
Kwa kuwa sisi watanzania tunaoishi nchini Uswidi, tumejiunga pamoja na kuamua kuanzisha baraza la kitaifa litakalo waunganisha diaspora, jumuiya na vikundi vya watanzania vyenye malengo sawa na baraza hili.
Na kwa kutambua kuwa umoja na ushirikiano ndiyo nguzo pekee itakayotuvusha na kutufikisha kwenye malengo yetu ya kiuchumi, kiutamaduni, kijamii na kimichezo. Tumeamua kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja kupitia baraza hili kwa lengo la kuhakikisha kuwa tunaweza kutatua changamoto zilizopo mbele yetu ili kufanikisha malengo hayo.
Hivyo basi kwa nia moja tumedhamiria kuanzisha umoja wetu wa Watanzania tunaoishi nchini Uswidi. Tukisisitiza umuhimu wa kuungana pamoja katika matukio mbali mbali yanayotuhusu sisi wanadiaspora watanzania na familia zetu. Baraza letu litawashirikisha pia wale wenye uzalendo na nchi yetu ya Tanzania na wenye maono yanayofanana na malengo ya kuanzisha baraza hili.
Att representera Tanzanier och Tanzaniska medlemsföreningar i Sverige. Att samordna, stödja och presentera medlemsföreningarnas arbete. Att bevara, utveckla och presentera den nationella, språkliga och kulturella identiteten inom ramen för ett multikulturellt svenskt samhälle. Att verka för enighet och samarbete bland Tanzanier och Tanzaniska föreningar i Sverige. Att upplysa Tanzanier om det svenska samhället. Att verka för Tanzanier med integration och anpassning i det svenska samhället genom information, möten, cirklar och seminarier. Att aktivt arbeta med åtgärder mot missbruk av alkohol och narkotika bland Tanzaniska ungdomar och informera dem om konsekvenserna av missbruket, genom t ex möten, film, muntlig och skriftlig information. Att främja jämställdhetsarbete Att engagera sina medlemmar i fred och antirasistiska rörelser och verka för förebyggande åtgärder mot diskriminering. Att arrangera seminarier, konferenser, cirklar, föreläsningar och utställningar om Tanzania kultur och följa upp alla utvecklingar både här i Sverige och Tanzania Att samarbeta med andra svenska och etniska organisationer och svenska myndigheter för förverkligandet av förbundets målsättningar. Att informera svenskar och svenska myndigheter om Tanzanier, Tanzanisks kultur, språk, historia. Att informera medlemsföreningar och svenska myndigheter om situationen och utvecklingen i Tanzania, Att sprida Tanzanisks mat, kultur och språket. Att skapa utvecklingsmöjligheter för de Tanzaniska barnen i Sverige samt stimulera ungdomarna till högre utbildning. Att ordna utflykter och sommarläger för medlemmarna. Att ordna Tanzaniska konserter och fester för både Tanzanier och Tanzanier vänner. Att verka för de Tanzaniska barnen får hemspråksundervisning genom sina lokala föreningar. Att verka för utveckling och ökning av de lokala föreningarna inom landets kommuner och vara behjälplig vid start av nya föreningar.
Kuwawakilisha watanzania na Jumuiya wanachama wa Umoja huu hapa Uswidi. Kuratibu, kusaidia na kutambulisha kazi za Jumuiya wanachama wa Umoja huu. Kutunza, kuendeleza na kutambulisha sura ya Taifa, lugha na utamaduni wa Kitanzania ndani ya jamii ya Uswidi inayojumuisha tamaduni nyingi. Kuimarisha umoja na ushirikiano baina ya Watanzania na Jumuiya za Watanzania zilizopo nchini Uswidi. Kuwajuvya (kuwapa maelezo) Watanzania juu ya jamii ya Uswidi. Kuwasaidia Watanzania waliopo Uswidi kwa ujumla na hususan wakimbizi kutoka Tanzania juu ya masuala ya kijamii na kuwapa maelezo juu ya haki zao na wajibu wao katika jamii ya Uswidi. Kutenda kazi ya kuwaunganisha Watanzania sambamba na kukidhi haja ya uwiano na jamii ya Uswidi kwa kupitia taarifa, mikutano, kozi fupifupi kwa mfumo maalum na semina. Kushiriki kikamilifu katika kuchukua hatua mbalimbali juu ya matumizi mabaya ya pombe na madawa ya kulevya miongoni mwa vijana wa Kitanzania, kwa kuwahabarisha juu ya athari za matumizi hayo – mfano kupitia mikutano, filamu, maelezo ya mdomo au kwa maandishi. Kuwahamasisha wanachama katika harakati za kujenga amani na kupinga ubaguzi wa kikabila na kujishughulisha katika harakati za kuzuia ubaguzi wa aina mbalimbali. Kuandaa semina, mikutano, kozi fupifupi kwa mfumo maalum, mihadhara na maonyesho kuhusu tamaduni za Tanzania na ufuatiliaji wa maendeleo mbalimbali – hapa Uswidi na Tanzania. Kushirikiana na vyama mbalimbali vya Uswidi, vya wageni-wakazi na mamlaka mbalimbali za Uswidi katika ufanikishaji wa malengo ya Umoja huu. Kuwahabarisha Waswidi na mamlaka mbalimbali za Uswidi kuhusu Tanzania, tamaduni zake, lugha na historia yake. Kuzihabarisha Jumuiya wanachama na mamlaka mbalimbali za Uswidi kuhusu hali na maendeleo nchini Tanzania. Kueneza ufahamu kuhusu vyakula vya Kitanzania, tamaduni na lugha. Kujenga misingi ya maendeleo kwa watoto wa Kitanzania hapa Uswidi na pia kuchochea hamu ya vijana kujiendeleza kielimu – elimu ya juu zaidi. Kuratibu safari za kimatembezi na kambi mahsusi za majira ya joto kwa ajili ya wanachama. Kuratibu maonyesho ya Kitanzania na tafrija mbalimbali kwa ajili ya Watanzania na marafiki wa Watanzania. Kufanya jitihada kwa ajili ya watoto wa Kitanzania waweze kupata mafunzo ya lugha ya Taifa kwa kupitia Jumuiya zao zilizo jirani na makazi yao. Kufanya jitihada kwa ajili ya kuendeleza na kuongeza idadi ya Jumuiya ndogondogo zilizoko ndani ya Manispaa zilizopo nchini Uswidi na pia kutoa usaidizi katika kuanzisha Jumuiya zingine mpya.