MKUTANO MAALUMU WA TANRIKS KUJADILI MIRATHI KWA
DIASPORA NA WAGENI KISHERIA.
Baraza la diaspora wa Tanzania Sweden -Tanriks linawakaribisha wanachama na diaspora wote na familia zao, katika mkutano maalumu wa kujadilia haki za diaspora za urithi kupitia sheria ya mirathi ya Tanzania. Katika mkutano huo wanasheria wataufahamisha umma tafsiri ya mahakama kuhusu haki ya mirathi kwa mali zisizoamishika na haki nyingine kwa diaspora na familia zao lakini pia wageni wasiokuwa raia wa Tanzania.
Mkutano utafanyika siku ya Jumapili tarehe 14 August 2022, kuanzia saa 10 -12 jioni saa za Tanzania ambapo ni sawa na saa 9 – 11 Jioni saa za Sweden. Watoa mada watakuwa ni Mwanasheria Alevander J. Barunguza na Mwanasheria Zakaria Maseke kutoka Tanzania. Nafasi ya kuchangia na kuuliza maswali kwa washiriki itakuwepo, washiriki mnaombwa kujiunga dakika 15 kabla ya muda wa mkutano ili tuweze kuanza na kumaliza kwa wakati uliopangwa.
Kwa msaada zaidi kuhusu mkutano huu WhatsApp namba +46724511963. Taariza zaidi za kushiriki zinapatikana hapa chini, na kwenye tangazo hapo juu. Kwa barua rasmi bonyeza hapa. MIRATHI KWA DIASPORA NA WAGENI KISHERIA Wote mnakaribishwa.
MKUTANO WA TANRIKS NA DIASPORA WOTE
MADA: MIRATHI KWA DIASPORA NA WAGENI. KISHERIA
SIKU: JUMAPILI TAREHE 14 AUGUST 2022.
MUDA: TANZANIA SAA 10 – 12 JIONI. SWEDEN: SAA 9 – 11 JIONI
MAHALI: CLUBHOUSE. JINA: TANRIKS DIASPORA
KUSHIRIKI: BONYEZA LINK HII – https://bit.ly/3oJzqNz (KISHA BONYEZA ALAMA YA KALENDA ILI UWEZE KUKUMBUSHWA SIKU YA MKUTANO. )
WAZUNGUMZAJI. WANASHERIA WAWILI WALIOBOBEA KTK SHERIA ZA MIRATHI. UPATAPO TAARIFA HII, MTUMIE DIASPORA MWENZAKO.
TANRIKS INAWALETA WATU WOTE PAMOJA
Adolph N. Makaya
Katibu Mkuu
TANRIKS
2022 08 08
1 Comment
Merina Paul
I’m grateful for this enables people to be aware of legal issues